Jumatatu , 19th Jan , 2026

Taita Mr II Sugu amerejea salama Tanzania akitokea nchini South Africa alipokuwa akipatiwa matibabu ya afya yake!

Picha ya Mr II Sugu

Sugu amewashukuru Madaktari wote waliookoa maisha yake na kumpa ruhusa ya kuendelea na maisha yake ya kawaida.

"Haya nimerudi salama Bongo namshukuru sana Mungu, Madaktari bingwa wote watatu walionitibu (wakiwemo Wayahudi wawili) wamesema sasa niko fit kuendelea na mishe zangu".

"Asanteni sana kwa maombi na ‘mitusi’ yenu pia cha msingi sijafa bado" ameandika Mr II Sugu.