Pichani Harmonize,Ibraah na Tundaman
"Harmonize naongea karibia kila siku na mara kadhaa nakutana naye, kitu kikubwa ni kwamba Konde kwa Ibraah hana ubaya naye na ameamua kuendelea'' Ameandika Tundaman
''Mimi kuna ngoma nimefanya na Ibraah kuna siku nikamuuliza kabla hajatoa Friendzone nikamuuliza kama naweza itoa akasema ngoma ni kali niitoe na akanijibu hata yeye kuna ngoma amefanya naye ataitoa (ambayo ni Friendzone) kwahiyo hata suala la video hiyo nikilifikisha inaweza ikafanyika'' Ameandika Tundaman
"Kwasababu kwa yeye hana kinyongo chochote na Ibraah sasahivi yeye kaamua kuendelea kufanya mambo yake na Konde hana kinyongo na Ibraah kuhusu video nitaongea nao" Ameandika Tundaman






