Alhamisi , 19th Mar , 2020

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa fedha za noti zimetengenezwa kwa namna ambayo zinaweza kuzuia vimelea kusalia, ikiwatoa hofu wananchi katika kipindi hiki cha kusambaa kwa virusi vya Corona. 

Pesa za noti za Tanzania

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Machi 19, imetoa ushauri kuwa kwakuwa noti hizo zinapitia katika mikono ya watu wengi, inawashauri wananchi kuzingatia miongozo inayotolewa na mamlaka zenye dhamana, ikiwa pamoja na kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (Sanitizer).

Aidha wananchi wanashauriwa kufanya miamala kwa kutumia njia mbadala za malipo kama vile simu za mkononi, intaneti na kadi bila kulazimika kufika kwenye kaunta za benki au ATM kuchukua noti.

Kama ilivyotangazwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa wa Corona ni tishio duniani kote na tayari umeingia nchini tangu Jumatatu, Machi 16, 2020.

Taarifa kamili hapa chini.