Bibi aliyeua mwanafunzi, auawa na wananchi

Alhamisi , 18th Apr , 2019

Mwanamke mmoja, Bi Coretha Francis mkazi wa kijiji cha Ihunga, kata ya Kishanda wilayani Muleba mkoani Kagera ameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali, baada ya kumtuhumu kuhusika na mauaji ya mtoto.

Picha za tukio hilo

Bi Coretha alituhumiwa kumuua mwanafunzi Ismail Hamis (7) ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho. 

Mbali na mauaji hayo, pia wananchi wamefyeka shamba la migomba la bibi huyo na kisha kuteketeza kwa moto nyumba yake.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka April 5 mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi leo mwili wake ulipogundulika umezikwa katika shamba la bibi huyo, akiwa na sare zake za shule.

Aidha Kamanda Revocatus amesema Taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika.