Jumatano , 2nd Jan , 2019

Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya ambaye pia ni Waziri Kivuli Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira ameendelea kushikilia msimamo wake wa kumtaka kujiuzulu kwa Waziri Jenister Mhagama kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Rais Magufuli juu ya hatma ya kikotooo kwa

Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya.

wafanyakazi ambao ni wastaafu.

Kwa mujibu  Bulaya, suala la kikokotoo limepelekea kushuka kasi ya utendaji kazi kwa baadhi ya taasisi nchini, lakini amedai suala hilo lilikuwa likipigiwa kelele na viongozi mbalimbali wa vyama vya upinzani wakiwemo wabunge.

"Hili jambo si sawa, tunatengeza mazingira ya kuwalinda wanasiasa. Kwahiyo Rais Magufuli amfukuze kazini au Waziri mwenyewe ajiuzulu kwa sababu yeye ndiye aliyetunga hizi kanuni," amesema Bulaya.

"Viongozi tuwe na utaratibu wa kukiri tunapokosea kwasababu mchakato wa sheria huwa unaanzia mbali sana, Waziri alikuja kukisema bungeni ambacho kilijadiliwa na kwenye baraza, kwahiyo ni bora angewawajibisha wote na si mtendaji peke yake," ameongeza Bulaya.

Hii ni mara ya pili kwa Mbunge huyo wa Bunda Mjini kutaka Waziri Jenister Mhagama kutoka kwenye nafasi yake ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kuahirisha matumizi ya kanuni mpya.