Alhamisi , 17th Jul , 2014

Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG Ludovick Utouh amemuita ofisin kwake mbunge wa kigoma kusini David Kafulila akimtaka apeleke ushahidi kuhusu tuhuma za ufisadi wa kampuni ya Independent Power Tanzania ltd (IPTL).

Mkaguzi na Mdhibiti mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania CAG Ludovick Utouh.

Kuitwa kwa Kafulila kumekuja ikiwa ni siku tatu tu tangu IPTL ilipomfungulia mashtaka mbunge huyo kwa tuhuma alizozitoa za wizi wa pesa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Kwa upande wake mbunge huyo wa kigoma kusini amekiri kupokea barua kutoka kwa CAG ya kuitwa kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma hizo.

Wakati huohuo, serikali imetakiwa kupanga viwango bora vya kodi kwenye bidhaa vitakavyoweka mazingiria bora ya kuendesha viwanda nchini.

Akizungumza jana jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la viwanda Tanzania (CTI)Leodegar Tenga amesema sekta ya viwanda nchini kwa kiasi kikubwa ina changamoto nyingi zinazotakiwa kufanyiwa kazi likiwemo suala la upangaji wa kodi kwenye bidhaa.

Tenga ameongeza kuwa duniani kote sulala la kodi kwenye bidhaa linapewa kipaumbele ili kuhakikisha kuwa serikali haiviumizi viwanda.