Jumatatu , 12th Oct , 2015

Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kuwa kitahakikisha reli ya kati inaimarishwa ili bandari kuu iliyopo eneo la Isaka wilayani kahama mkoani Shinyanga iweze kufanya kazi kwa ukamilifu na kuongeza ajira wananchi wa eneo hilo.

Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Mkoani Shinyanga

Akizingumza katika mikutano ya hadhara tofauti katika mkoa huo mgombea mwenza wa chama hicho Bi. Samia Suluhu amesema ilani ya chama hicho inazungumzia maboresho ya reli katika kuleta maendeleo ya watu wa kanda hiyo.

Bi. Samia amesema tatizo la bandari hiyo wanalifahamu ambapo hapo awali ilikua inatoa ajira mpaka watu elfu sita lakini kwa sasa imeshuka kiasi ambacho imesababusha viajana wengi kukosa ajira.

Katika hatua nyingine Bi. Samia amesema pia serikali ya chama cha mapinduzi itawaboreshea hali ya ufanyaji biashara wajasiriamali wadogo ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kunufaika nayo.