CCM yajiongezea idadi ya wabunge,yanyakua Masasi

Jumatatu , 21st Dec , 2015

Chama cha Mapinduzi kimeweza kutetea jimbo lake la Masasi katika uchaguzi ulifanyika jana baada ya kuahirishwa Okt. 25 mwaka huu kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea jimbo hilo kupitia chama cha NLD, Dkt. Emamanuel Makaidi kufariki Dunia.

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Masasi ambaye pia ni Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Masasi Fortunatus Mathew Kagoro.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na mkurugenzi wa halmashauri ya jimbo la Masasi Fortunatus Kagoro amesema kuwa Bw, Rashid Chuachua amepata kura 16,597 akifuatiwa na Ismail Makombe maarufu kama Kundambanda wa CUF, aliyepata kura 14,019.

Wengine walioshiriki katika uchaguzi huo ni Swaleh Ahmad wa CHADEMA, aliyepata kura 512, Omary Timothy wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 347, na Angelus Thomas wa NLD aliepata kura 70.

Wakati huo huo katika harakati za Uchaguizi wa Ubunge katika jimbo la Ludewa Wafuasi watatu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Jimbo la Ludewa wameshambuliwa na watu wanao daiwa kuwa ni wafusai wa chama cha Mapinduzi CCM na jeshi la polisi lina washikilia wafuasi saba kuhusiana na tukio hilo lililotokea usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbrod Mutafungwa kuthibitisha tukio hilo amesema kuwa jeshi hilo limewakamata na kuwahoji wafuasi saba wa CCM.

Hata hivyo katika Jimbo baada ya kufanyika uchaguzi matokeo ya awali yanaonyesha Deo Ngalawa wa CCM, ameongoza katika vituo vingi lakini hadi jana jioni matokeo yalikuwa hayajatangazwa.