Jumapili , 20th Mar , 2016

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Bw.

Msemaji wa CCM Christopher Ole Sendeka akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani.

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Mjumbe Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa msemaji wake.

Katibu Mkuu wa CCM Bw. Abdulrahmnan Kinana amesema Sendeka atafanyakazi zake chini ya Katibu wa NEC, Itikadi na Unezi Nape Nnauye.

Bw. Kinana amesema CCM imefanya uamuzi huo li kumuwezesha Nape kutekeleza majukumu yake ya Uwaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni Sanaa na Michezo.

Akitoa taarifa baada ya uteuzi huo Sendenka alikuwa na haya ya kueleza:-
Machi 15, 2016, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akiwaapisha Wakuu wapya wa mikoa, aliagiza pamoja na mambo mengine, viongozi katika ngazi mbalimbali kuhakikisha wanasimamia nguvu kazi ya vijana katika maeneo yao ili waache kukaa kijiweni.

Agizo hilo lililenga utekelezaji wa vitendo wa matumizi bora ya rasilimali watu nchini wakiwemo vijana ambao ni nguvu kazi muhimu kwa taifa, kujengewa mazingira mazuri yatakayowawezesha kujiajiri katika shughuli za uzalishaji mali.Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinampongeza kwa dhati Rais Magufuli kwa agizo lake hilo lenye lengo muhimu la kuwafanya watanzania kwa pamoja kuwajibika.

CCM inampongeza Rais Magufuli kwani kwa mara nyingine tena amedhihirisha kuwa wapiga kura walio wengi walifanya uamuzi sahihi kwa kumchagua yeye kuwa Rais wa Serikali ya awamu ya Tano katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana.

CCM kama chama anachotoka Rais Magufuli na ambacho ndicho Ilani yake inatekelezwa na serikali kwa kupindi cha 2015/2020, ina kila sababu ya kumpongeza kwa kuanza vizuri katika uongozi wake wa miaka mitano na tunaamini kuwa katika kipindi hicho, “Tanzania Tunayoitaka” itafika mbali kimaendeleo kwenye kila ngazi.