
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Makene ametoa kauli hiyo leo Juni 23, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kueleza hali ya Mbowe kuwa anaendelea vizuri, lakini wamekuwa wakishangazwa na matokeo ya uchunguzi uliotolewa, huku wakidai kuwa na mashaka kwani uchunguzi hauko huru wala wazi.
"Bahati mbaya kila ukisikia kauli za Polisi bado wanaonekana wameshatengeneza points za kumshambulia na kumkandamiza muathirika wa tukio la kuvamiwa na kushambuliwa, na wanakuwa wako 'very bias' tunakosa hata uchunguzi wa uhuru unaofanywa na Polisi badala ya kujielekeza kupata ukweli wa tukio ili mwisho wa siku kukomesha vitendo hivi" amesema Makene.
Mbowe alishambuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 9, 2020, wakati akipandisha ngazi kuelekea nyumbani kwake Jijini Dodoma, ambapo baadaye taarifa ya Polisi ilitolewa na kuonesha kuwa siku ya tukio Mbowe alikuwa amelewa chakari.