Jumatatu , 21st Sep , 2015

Chama cha siasa cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana usiku kimezindua zoezi la uchangiaji fedha kwa ajili ya kampeni za uchaguzi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mgombea Urais kuptia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, chini ya Mwamvuli wa UKAWA Mh. Edward Lowassa akizungumza na Mwenyekiti wa chama hicho Mh. Freeman Mbowe

Hafla hiyo iliyohudhiriwa na mgombea urais wa Chadema Mh. Edward Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji fedha zilichangishwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kupitia mitandao ya simu, akaunti za benki pamoja na fedha taslim.

Akiongea katika hafla hiyo mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amewataka watanzania kuchangia mabadiliko kwa niaba ya watanzania na si kwa ajili ya Lowassa ama Mbowe.

Naye Mh. Lowassa na Duni wamewataka watanzania kuchangia kiasi chochote walichonacho kwani kutoa ni moyo si utajiri.