Ijumaa , 21st Jan , 2022

Aliyewahi kuwa mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, amempongeza mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson, kwa kuchaguliwa na Kamati Kuu ya CCM kuwa mgombea pekee wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Andrew Chenge

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 21, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio na kusema anaheshimu na ameridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na kupelekea kupatikana mwana CCM ambaye atapigiwa kura na wabunge wote ili kushika nafasi hiyo.

"Najua Spika wetu ajaye Tulia Ackson mimi nampongeza na nimtakie mema kwamba yajayo yanafurahisha," amesema Andrew Chenge.

Andrew Chenge, alikuwa ni miongoni mwa watu 71 waliojitokeza kuchukua fomu ya kuomba nafasi ya kuteuliwa kugombea kiti cha Uspika wa Bunge