
Tamko la China linakuja wakati duru za kimatibabu zikiliambia Shirika la Anadolu kwamba mashambulizi ya anga ya Israel yaliyolenga nyumba na mahema yaliyokuwa yakihifadhi Wapalestina waliokimbia makazi yao katika Jiji la Gaza, na maeneo ya kati na kusini mwa eneo la Palestina yakiwaua Wapalestina 12 mapema leo Jumatano Septemba 17.
Mauaji ya hivi punde yamekuja wakati jeshi la Israel lilipotangaza awamu mpya ya mashambulizi yake ya ardhini katika mji wa Gaza siku ya jana Jumanne kama sehemu ya mkakati mpana wa kuukalia tena mji mzima. Wakati huo huo Israel imetangaza njia mpya ya muda kwa wakazi wanaoukimbia mji wa Gaza, huku ikianzisha mashambulizi makali ya ardhini baada ya mashambulizi makubwa ya mabomu katika mji mkuu wa eneo la Palestina.
Jeshi la Israel pia, limetangaza kufunguliwa kwa njia ya muda ya usafiri kupitia Mtaa wa Salah al-Din, msemaji Avichay Adraee alisema katika taarifa, akiongeza kuwa njia hiyo itafunguliwa kwa saa 48 pekee.
Mashambulio mapya ya Israel katika mji wa Gaza ni ya kutisha, kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kanada ambayo imeongeza kuwa "Inazidisha mzozo wa kibinadamu na kuhatarisha kuachiliwa kwa mateka na kuitaka serikali ya Israeli kufuata sheria za kimataifa kwa mujibu wa wizara hiyo katika jukwaa la mtandao wa kijamii la Marekani la X.
Vikosi vya Israel vilivamia maeneo kadhaa ya Al Khalil (Hebron) katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu na kuwashambulia kinyama Wapalestina na kuharibu magari, liliripoti shirika la habari la WAFA. Vikosi hivyo vilivamia eneo la Al-Ras magharibi mwa Idhna na kitongoji cha Wadi al-Nasara, kwa mujibu wa shirika hilo.
Pia vilisimama kwenye lango la kambi ya wakimbizi ya Al-Fawwar, kusini mwa Al Khalil, walivunja vioo vya magari kadhaa yaliyokuwa yameegeshwa karibu na lango la kambi hiyo, shirika hilo lilisema.