Jumapili , 13th Sep , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amevikemea Virusi vya  Corona huku akivitaja kuwa ni moja ya sababu ya kuchelewesha utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta baina ya Tanzania na Uganda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanaznia, Dkt John Pombe Magufuli.

Magufuli amekemea virusi hivyo leo Septemba 13, 2020, wakati wa uwekaji wa saini wa mkataba  wa utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta, mbele ya Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni uliofanyika mkoani Geita, ambapo pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Museveni kwa uvumbuzi wa mafuta hayo.

"Mradi huu umechelewa, na bahati mbaya wakati wanaendelea kujadili pakatokea Corona na ishindwe na ikalegee huko, ikawa inachelewesha, nani anapenda kufa kwahiyo hili licorona likaanza kukoromela huu mradi wetu wa mafuta", amesema Rais Magufuli.

"Jana Mzee Museveni akanipigia simu ananiambia, pamoja na Corona ninaomba tumalizie huu mradi uanze, Corona isiwe sababu ya kuchelewesha maendeleo ya Watanzania na Waganda, akasema mimi nitakuja na barakoa nikamwambia njoo mradi haulali", ameongeza Rais Magufuli.