Jumapili , 26th Jan , 2020

Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama cha wananchi CUF, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Misima wilayani Handeni, Masoud Mhina amesema kuwa utaratibu uliopo kwa sasa ni kumuwekea dhamana Profesa Lipumba na baada ya hapo mwanasheria atatoa mwongozo.

Profesa Lipumba akipanda gari la polisi, baada ya kukamatwa.

Hayo ameyabainisha leo Januari 26, 2020, wakati akizungumza na EATV mara baada ya Mwenyekiti wa chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba kukamatwa na jeshi la polisi wilayani Handeni kwa kosa la kufanya mikutano bila kibali.

"Tupo kwenye mchakato wa kumwekea dhamana Profesa Lipumba na baada ya dhamana hiyo Mwanasheria wa Lipumba, atatoa muongozo wa hatua zinazotakiwa zichukuliwe" amesema Mhina.

Profesa Lipumba amekamatwa mapema leo Jumapili, katika kijiji cha Mbogoni kata ya Mgwe akiwa katika kikao cha ndani na wanachama wa chama hicho, katika moja ya nyumba ya mwanachama wa chama hicho.