
IGP Sirro, wakati akizungumza na wakazi wa Migori Iringa
IGP Sirro amesema hayo akiwa eneo la Migori mkoani Iringa wakati akizungumza na wananchi wa eneo hilo.
"Umemuoa mwanamke wako au hawara yako mnaishi pamoja, mkahitilafiana kuna sababu ya kutafuta visu unamchoma mwenzako unamuua, ebu Watanzania tufike mahala tubadilike huu ni ujinga, kama amekuzengua si unaachane naye, kwahiyo shida tunayopata sasa hivi mauaji mengi ni hayo hayo (Mapenzi)", amesema IGP Sirro
Aidha IGP Sirro ameongeza "Lakini akina dada pia uangalie na mwanaume gani unakaa naye, sio kila mwanaume ni bora kuna wanaume wengine mizigo, na kuna wanawake wengine mizigo si ndio eeh,".