
Yanga wakishangilia ubingwa wa NBC PL 2024/25
Yanga walifanikiwa kutetea ushindi wao mbele ya watani wao Simba hapo jana wakiwachakaza kwa kuwafunga magoli mawili kwa Sifuri, Penati ya Winga wao Machachari Pacome Zouzoua na Goli la dakika za jioni la Clement Mzize Liliwamaliza nguvu Simba na Yanga kuondoka na Ushindi wa 2-0
Baada ya kichapo hicho Yanga wamemaliza msimu wakiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi kuu ya NBC wakiwa na alama 82 huku watani zao Simba wakiwa na alama 79 katika nafasi ya Pili ikiwa ni nafasi nzuri zaidi ya msimu uliopita ambapo walimaliza nafasi ya 3, Azam FC wakishika nafasi ya Pili.
Mchezo wa Dabi ya Kariakoo ulikuwa ni mchezo uliokuwa na mivutano tangu kuahirishwa Machi 8 baada ya Simba kutofika uwanjani kwa madai ya kuzuiwa kuingia uwanjani kwaajili ya kufanya mazoezi ya mwisho, Yanga waligeuza kibao na kutoutambua tena hadi matakwa yao kutimizwa na ndipo walipokubali kushuka tena Dimbani Juni 25 baada ya matakwa yao kutimizwa.
Ushindi wa Yanga hapo jana unakamilisha idadi ya vichapo vitano mfululizo kwa watani zao Simba huku kipigo kikubwa Yanga wakiibuka na ushindi wa Magoli 5-1