daladala
Siku ya pili sasa madereva hao wamesitisha huduma hizo kwa kile wanachodai kuwa madereva bajaji wameshindwa kufuata utaratibu na kuingilia maeneo yao ya kusafirisha abiria katika Mji wa Njombe huku wakisisitiza kutorejea barabarani mpaka pale mamlaka zitakapozuia bajaji kuingia maeneo yao ya usafirishaji.
EATV imezungumza na msimamizi wa daladala mjini humo Seleman Malekela, pamoja na Mwenyekiti wa daladala Samweli Mvile ambapo wote kwa pamoja wameonekana kutoridhishwa na hatua hiyo iliyochukuliwa na madereva bajaji mjini humo.
Katibu Tawala wilaya ya Njombe Emmanuel George, amezungumza na madereva hao na kuwaomba kuendelea kutoa huduma wakati serikali ikiendelea kujadili namna ya kufikia ufumbuzi wa jambo hilo.
Kwa mujibu wa madereva daladala mjini Njombe, wameiomba serikali kuwazuia madereva bajaji kufika katika maeneo ya Kibena, Nundu na Hagafiro.
