Jumanne , 8th Mar , 2016

Mkoa wa Dar es salaamu unakabiliwa na Upungufu wa zaidi ya vyumba vya madarasa elfu tano pamoja na upungufu wa madawati elfu 68,na hivyo kusababisha wanafunzi wengi waliojiunga na masomo mwaka huu kukaa chini.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw, Said Mecky Sadick

Akiongea na Waandishi wa habari ofisini kwake jana Jijini Dar es Salaam Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Bw, Said Mecky Sadick amesema kutokana na hali hivyo wadau wametakiwa kujitokeza kuisaidia sekta ya elimu katika mkoa huo na nchi kwa Ujumla.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa lazima uongozi wa Mkoa upate ufumbuzi wa kudumu wa kutatua kero za elimu ikiwa ni pamoja na kujenga madarasa na shule mpya katika maeneo ya wazi.

Mecky Sadicky ametumia fursa hiyo pia kuwaonya watumishi ambao wanakimbilia kuuza viwanja huku wanafunzi wakiendelea kusoma nje pamoja na kukaa chini hivyo juhudi zinahitajika katika kulifuatilia suala hilo mtambuka.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amezungumzia ziara ya rasi wa Jamhuri wa Vietnam ambae atawasili nchini leo saa mbili na nusu usiku katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere JKN.