Mkuu wa wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa
Agizo hilo amelitoa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa hlamashairi ya jiji la Tanga ambapo Mgandilwa ameyataja maeneo hayo kuwa ni eneo la Sabasaba na barabara ya Uhuru na kusema kuwa wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo, amewataka wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo.







