Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kali amesema atawachukulia hatua za kisheria wafugaji wakorofi wanaolisha mifugo yao kwa makusudi kwenye mashamba ya wakulima kwa kuwaweka mahabusu kwa siku 10  ili iwe fundisho kwa wafugaji wengine wasioheshimu jasho la wakulima.

Mkuu wa Wilaya ya Magu Salum Kali

Kali ameyasema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyashimbi wilayani humo mkoani Mwanza lengo likiwa ni kutafuta ufumbuzi wa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

"Ng'ombe wa mfugaji wakiingia kwenye shamba na akawa jeuri kamata mwenye ng'ombe niletee ofisini kwangu OCD atamuhifadhi kwa maelekezo yangu na ntampeleka kwenye kambi ya gereza akae siku kumi ndo tumtoe aende mahakamani, sitakubali na hii iwe fundisho kwa mfugaji yeyote katika wilaya yangu ya Magu" amesema DC Salum

Kwa upande wa wakulima wamebainisha changamoto iliyopo baina yao na wafugaji ni kutokuheshimiana kwenye kazi zao ilihali wao ni kama mtu na mdogo wake.