Dereva aliyekaidi kusimama baada ya kusimamishwa na Trafiki
Naibu Waziri Sagini ametoa kauli hiyo huku akiagiza wataalamu wa afya kuhakikisha wanawapima afya ya akili madereva.
"Nimeona clip ya dereva wa gari ndogo Trafiki wangu anamsimamisha yeye anampelekea gari, hivi huyo bado yuko barabarani?, akamatwe apelekwe kwenye vyombo vya dola, na leseni yetu anyang'anywe, wakati mwingine Trafiki akikuzuia anataka kukuokoa, mimi nina wasiwasi na akili za madereva wetu," amesema Naibu Waziri Sagini

