Alhamisi , 7th Jan , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.

Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Aidha Rais huyo Mstaafu amesema kazi za marais wastaafu ni kumpa moyo Rais na kumuunga mkono na kusema kuwa hakuna nchi ambayo inaendeshwa bila ukusanyaji wa mapato hivyo kazi waliyoianza viongozi wa serikali ya awamu ya tano imeanza vizuri na akiwataka waendelee kufanya hivyo.