Jumanne , 30th Mei , 2023

Makamu wa Tanzania Dkt Philip Mpango ameiagiza wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kukamilisha ujenzi wa Barabara yenye miundombinu korofi ya Ngaresero - Engaruka Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha yenye urefu wa Kilometa thelathini na tisa kwa kiwango cha Lami

Makamu wa Rais Dkt Mpango ametoa maagizo hayo wakati akizundua barabara ya Waso hadi Sale yenye urefu wa Kilometa 49 iliyoghalimu zaidi ya bilioni themanini na saba. Na kuitaka wizara kuzingatia zaidi maeneo yenye changamoto katika ujenzi na ukarabati huo.

 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Geofrey kasekenya anakiri ubovu wa miundombinu duni kwenye barabara hiyo, na hapa anaeleza mpango wa Wizara. 

Kwa upande mwingine Makamu wa Rais amewasha taa katika kijiji Cha Sale kama ishara ya kukamilika Kwa mradi wa Umeme kijijini humo,mradi uliotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini REA. na hapa anatoa maelekezo kwa Wizara ya nishati. 

Nao baadhi ya wakazi wa kijiji cha Salé wameishukuru Serikali kwa kuwafikishia Huduma ya nishati ya umeme kijijini humo, na kuwa kilikuwa kilio cha muda mrefu Kwa wakazi hao