Jumanne , 13th Jan , 2015

Katibu  Mkuu   wa  Jumuiya  ya  Afrika  Mashariki  Dkt  Richard  Sezbera  amesema  jumuiya  hiyo  imefanikiwa  kwa  kiasi  kikubwa   kukabiliana  na  changamoto   za  kisiasa  kiuchumi  na  kijamii  na  malengo  yaliyowekwa   yanaendelea  kufikiwa

Sezbera  amesema  pamoja   na  tatizo  la  uhaba  wa  fedha  linaoikabili  jumuiya  hiyo  imefanikiwa  kwa  kiasi  kikubwa   kukabiliana  na  changamoto   za  kisiasa  kiuchumi  na  kijamii  na  malengo  yaliyowekwa   yanaendelea  kufikiwa  likiwemo  la  kupunguza  kutegemea  misaada  toka  kwa  wahisani.

Akizungumzia  hatua  iliyofikiwa  katika  utekelezaji  wa  malengo  ya  jumuiya  hiyio  katika  kipindi  cha  mwaka  2014/2015  Dkt Sezbera  amesema  utegemezi  wa wahisani  unaendelea  kupungua  na  uchumi  na  ushirikiano  unaimarika  kwa   nchi  wanachama  na  kwa  wananchi   kwa  ujumla .

Kuhusu changamoto  za kisiasa  ikiwemo  ya  vuguvugu  la  uchaguzi  linalozikabili  nchi  za  Burundi  na  Tanzania   Dkt. Sezbera  amesema   ni  za  kawaida  na  pia  jumuiya  inaendelea  kushirikiana  na  nchi  husika  kuhakikisha  inafanya kila  linalowezekana  kuhakikisha   kuwa  changamoto zote  zinazojitokeza  zinatatuliwa kwa njia  ya mazungumzo .

Akizungumzia  hatua  iliyofikiwa  katika  kuimarisha  uchumi  dr, sezbera  amesema  pamoja  na  kuwepo  kwa  changamoto  katika  sekta  za  mbalimbali  za  uchumi  ikiwemo  ya  utalii  amesema  jitihada  zinaendelea  na  baadhi  zimeshapata ufumbuzi  na  zingine  zinaendelea  kutafutiwa  majawabu .

Akizungumzia  suala  la  usalama  Dkt Sezbera  amesema  hali  ni  shwari  na jitihada  za  kuhakikisha  kuimarisha  utulivu  na amani  katika  nchi  wanachama  na  majirani  zake  ikiwemo  nchi  Sudani  Kusini  zinaendelea  sambamba  na mazungumzo  ya     kuiwezesha  nchi hiyo  kujiunga a na  jumuiya.