Shirika habari la Korea Kaskazini limesema kwamba kiongozi wa nchi hiyo Kim Joung Un, amefanya ziara yake katika eneo la magharibi la Nampo siku ya Jumanne na Jumatano, ambapo kwenye ziara hiyo alikagua ujenzi wa meli ya tatu ya daraja sawa na meli yake ya kivita ya tani 5,000, Choe Hyon, iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza Aprili 2025.
Kim amesifu maendeleo ya ujenzi wa meli hiyo kama maendeleo makubwa kuelekea lengo lake la kupanua wigo wa uendeshaji na uwezo wa kushambulia wa kijeshi wake wenye silaha za nyuklia.
Vyombo vya habari vya serikali vinasema kuwa meli hiyo imeundwa kushughulikia mifumo mbalimbali ya silaha, ikiwa ni pamoja na silaha za kupambana na anga na za majini, pamoja na makombora yenye uwezo wa nyuklia.



