Jumatano , 1st Jul , 2015

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji EWURA jana imezitaja bei mpya elekezi ya rejareja ya mafuta licha ya bidhaa hiyo kushuka bei katika soko la Dunia.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa nishati, maji nchini Felix Ngalamgosi akizungumza na waandishi wa habari.

Taarifa iliyotelewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura Felix Ngamlagosi ilitaja bei hizo mpya zitakazoanza kumika kuanzia leo kuwa ni Petrol iliyongezeka kwa sh. 232 kwa lita sawa na asilimia 11.82, dizeli imeongezeka kwa shilingi 261 kwa lita sawa na asilimia 14.65 na mafuta ya taa yameongezeka kwa sh. 369 sawa na asilimia 22.75.

Ngamlagosi alizitaja kati ya sababu zilizosababisha kuongezeka kwa mafuta ni kuendelea kudhoofu kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani na pia mabadiliko ya tozo za serikali katika mafuta kuanzia hii leo.

Taarifa ya EWURA ilieleza kuwa kufuatilia mabadiliko hayo bei elekezi kwa rejareja ya Petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam ni sh. 2,198, dizeli sh.2043 na mafuta ya taa ni shilingi 1993.

Kulingana na thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani kwa machapisho ya bei za mwezi Juni na Julai 2015, shilingi imepungua thamani kwa shilingi 175.11 kwa dola ya Marekani sawa na asilimia 8.65.