Jumatatu , 27th Jan , 2020

Kesi ya uhujumu uchumi namba 75 ya mwaka 2019, inayomkabili Mwandishi wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera, imesogezwa mbele hadi Februari 10, 2020, kwa madai ya kuwa upelelezi bado haujakamilika na kwamba mtuhumiwa bado anafanya majadiliano na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini.

Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Hayo yamebainishwa leo Januari 27, 2020, na Wakili wa Serikali, Gloria Mwenda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kawa ajili ya kutajwa.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu, ikiwemo kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi pamoja na utakatishaji wa pesa zaidi ya shilingi milioni 170, matukio ambayo anadaiwa kuyatenda maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.