Jumatano , 17th Sep , 2025

Fidia hiyo inakuja kufuatia vifo 72 vilivyotokea katika maandamano hayo yaliozuka Septemba 7, 2025 kutokana na marufuku ya mitandao ya kijamii, ufisadi wa baadhi ya viongozi na hali ngumu ya maisha kwa vijana wa taifa hilo.

Serikali ya Nepal imetangaza kutoa rupia 1.5 milioni ambazo ni sawa na Shilingi Milioni 42 kwa ajili ya fidia kwa familia za wafiwa waliofariki katika maandamano ya GenZ yaliotokea nchini humo wiki chache zilizopita.

Fidia hiyo inakuja kufuatia vifo 72 vilivyotokea katika maandamano hayo yaliozuka Septemba 7, 2025 kutokana na marufuku ya mitandao ya kijamii, ufisadi wa baadhi ya viongozi na hali ngumu ya maisha kwa vijana wa taifa hilo.

Fedha hizo zitagawanywa kupitia Ofisi za Tawala za Wilaya, ili kufikia familia za wafiwa ambao wengi walikuwa vijana waliojitokeza kwa wingi katika maandamano hayo yaliyomng’oa madarakani waziri mkuu KP Sharma Oli.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Om Prakash Aryal, amesema ofisi za umma zitapeperushwa bendera nusu mlingoti leo Septemba 17, 2025 ambayo pia ni siku ya maombolezo ya kitaifa kama ishara ya kuwakumbuka waliofariki kwenye maandamano hayo.