Basi la Frester lililopata ajali mkoani Shinyanga
Ajali hiyo imetokea leo Desemba 17, 2020, majira ya saa 12:00 asubuhi, katika eneo la Nyakato nje kidogo ya mji wa Kahama, likiwa kwenye mwendokasi muda mfupi tu baada ya Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini, Wilbroad Mutafungwa, kulikagua basi hilo na kuliruhusu kuendelea na safari.
Kamanda Mutafungwa, alikutana na madereva wa mabasi yote yaendayo mikoani kabla ya kuanza safari na kuwakumbusha kuzingatia sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kutoendesha kwa mwendokasi.
"Haiwezekani upatiwe elimu ya usalama barabarani halafu muda huo huo ukiuke sheria na kusababisha ajali huu ni uzembe,kwani amesababisha kifo na kujeruhi watu 23 tutachukua hatua kali dhidi yake pindi atakapokamatwa", amesema Mutafungwa.
Aidha Kamanda Mutafungwa, ameongeza kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 47 ambapo 23 wamejeruhiwa na watatu hali zao sio nzuri huku wengine wakiruhusiwa kuendelea na safari baaada ya kupata michubuko ambapo kampuni hiyo ililazimika kuwatafutia usafiri mwingine na kuendelea na safari kwenda mkoani Mara.





