Gesi itapunguza kiwango cha umaskini - Utafiti

Jumatano , 4th Jun , 2014

Utafiti unaonesha kuwa asilimia 55 ya wananchi wa Tanzania wanaamini kuwa rasilimali ya gesi na mafuta yatalinufaisha taifa, huku asilimia 45 wakiamini kuwa serikali na matajiri ndio watakaonufaika.

Picha ya mgodi wa gesi.

Takwimu hiyo imetolewa na taasisi ya Twaweza kwakushirikiana na banki ya dunia na umetokana na sauti za wananchi na ndio utafiti wa kwanza Afrika kwa njia ya simu wenye uwakilishi wa kitaifa.

Utafiti huo unaonyesha pia matakwa ya wananchi sawa na asilimia 20 yanataka kiasi cha mapato ya mafuta na gesi kipelekwe moja kwa moja kwa wananchi.