Jumatano , 16th Mei , 2018

Baada ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Nchini Abdul Nondo kuandikia mahakama barua ya kumkataa Hakimu anayeendesha kesi yake ajitoe kwa kuwa anamtilia mashaka, Hakimu wa huyo amegoma kujitoa katika kesi hiyo kwa maelezo kuwa malalamiko ya mshtakiwa hayana ushahidi wa kutosha.

Akitoa uamuzi huo mdogo wa Mahakama, John Mpitanjia amesema mahakama ni chombo cha mwisho cha kutenda haki hivyo itaangalia usawa kwa pande zote mbili ikiwa ni sambamba na kutoa haki kwa wakati bila kufungamana na upande wowote.

Siku ya Mei 15, 2018 Nondo aliiandikia baruaMahakama hiyo ya Wilaya ya Iringa, kumkataa hakimu huyo anayesikiliza shauri lake, kwamba anamtilia shaka na ameona aiandike barua Mahakama ili itende haki.

Nondo ambaye anashtakiwa kwa makosa mawili ya kudanganya kutekwa na kutoa maelezo ya uongo kituo cha Polisi Mafinga, alisema kuwa haridhishwi na mwenendo wa kesi yake na anazo hoja 5 ambazo ameziwasilisha mahakamani hapo kuomba kubadilishwa kwa hakimu.

Ali amekuwa akimuona Hakimu Mpitanjia akiwa na RCO wa wakiwa ofisini na kupanda gari lake jambo ambalo limepelekea yeye kuhisi kwenda tofauti na kesi yake Mahakamani hapo.

Baada ya kutoa uamuzi huo hakimu aliamuru upande wa Jamuhuri kuendelea kutoa ushahidi wa mashahidi waliobaki katika kesi hiyo.