Jumatatu , 13th Feb , 2023

Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita, amesema kwamba kiuhalisia hakuna ajali ya ndege ya abiria iliyotokea wilayani humo na kwamba kilichofanyika leo ni zoezi la utayari wa kukabiliana na ajali za aina hiyo lililoandaliwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

Ndege ya majaribio

DC Mboni ametoa kauli hiyo hii leo Februari 13, 2023, wakati akizungumza na East Africa TV & East Africa Radio Digital, mara baada ya taarifa kusambaa mitandaoni zikionesha kwamba kuna ajali ya ndege imetokea na kuua watu wapatao 10, majeruhi 23 na walionusurika ni 9.

"Lilikuwa ni zoezi la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ambalo huwa wanalifanya kila baada ya miaka miwili kuweza kujipima utayari wa kuokoa iwapo itatokea dharura ya aina yoyote, hili zoezi ili liende sawia lazima waweke scenario, kiuhalisia hakuna vifo vilivyotokea wala majeruhi," amesema DC Mboni Mhita.

Tazama video hapa chini