Jumamosi , 4th Jul , 2020

Wanafunzi watatu katika shule ya sekondari Islamic ilipo ilala Jijini Dar es Salaam wamefariki dunia kufuatia ajali mbaya ya moto ulizuka majira ya saa nane za usiku ukianzia katika mabweni wa shule hiyo.

Sehemu ya mabweni yaliyoungua

Akizungumza na waandisha wa habari akiwa katika eneo la tukio mapema leo, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Bi Sophia Mjema amesema moto huo ulianza kuwaka usiku na jitihada zilizofanywa zilifanikiwa kuwaokoa wanafunzi wengi lakini bahati mbaya wanafunzi watatu walikutwa wamepoteza maisha.

Mkuu huyo wa wilaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama amesema chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana ingawa tayari ameunda kamati ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Hata hivyo mkuu wa wilaya ameruhusu watoto kwenda kusoma kwa muda katika shule za jirani ili wasikose masomo lakini pia serikali kwa kushirikiana na uongozi wa shule kuweka mazingira mazuri ya kusomea katika kipindi hiki cha mpito.

Naye Shekh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema anaichukulia ajali hiyo kama janga hivyo kama kiongozi wa dini anatoa pole kwa uongozi wa shule serikali na familia za watoto waliokumbwa na ajali hiyo.