Alhamisi , 21st Jul , 2016

Mkutano wa 14 wa UNCTAD ukiwa umeingia siku ya Nne, mjini Nairobi, Kenya, nchi wanachama wa kamati hiyo zimekuwa zikijadili makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi, EPA huku Tanzania ikisisitiza kuwa haitasaini mikataba ikiwa imefumba macho.

Suala la mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi, EPA limekuwa likipatiwa kipaumbele katika mkutano wa 14 wa UNCTAD, ikielezwa kuwa ni moja ya njia za kuwezesha nchi zinazoendelea kujikwamua kutoka umaskini.

Hata hivyo kutoka nchi zinazoendelea kumekuwepo na wasiwasi pengine ni mtego na katika kusaini mikataba hiyo kumekuwepo na kusuasua ambapo Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Charles Mwijage, amesema kamwe hawataweza kusaini mikataba wakiwa wamefumba mambo kwa kuwa wanahitaji ufadhili.

Aidha Mhe. Mwijage amezungimzia msimamo wa Tanzania kuhussu mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Muungano wa Ulaya, EU na kusema kuwa Tanzania imesitisha ushirikiano huo mpaka pale itakakapojiridhisha na ushirikiano huo

Mkataba wa EPA kati ya EU na EAC ulikuwa utiwe saini Julai 18 mwaka huu.

Sauti ya Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Charles Mwijage,