Amesema miradi ya wananchi, vituo vya polisi, magari na biashara zilichomwa moto kwa makusudi na hivyo hatua zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi na usalama zilikuwa halali kulingana na ukubwa wa tukio.
“Vurugu si maandamano. Serikali ina jukumu la kulinda wananchi na mali zao. Hatuwezi kuruhusu watu wachache kujaribu kuivuruga nchi kwa visingizio vya maandamano,” alisema Dkt. Samia.
Ametoa wito kwa Watanzania kutambua thamani ya amani na kutokubali kutumiwa kama chombo cha vurugu, huku akisisitiza kuwa dola haiwezi kusubiri kuvamiwa ndipo ichukue hatua.



