Alhamisi , 30th Sep , 2021

Mfanyabiashara wa duka la simu mkoani Katavi Issa Kasili, amemfumania rafiki yake Mayombi Mwela, ambaye ni mfanyabiashara wa zao la mpunga katika Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele mkoani humo kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na mke wake.

Mayombi Mwela akiwa na mke wa rafiki yake baada ya kufumaniwa 'Guest house'

Taarifa zimeeleza kuwa baada ya Mayombi kufumaniwa, rafiki yake huyo alimtaka kumlipa faini ya pesa kiasi cha shilingi milioni 5, kiasi ambacho alikilipa bila pingamizi yoyote.

Kupitia mitandao ya kijamii kuna video inasambaa ikimuonesha Mayombi alivyofumaniwa, na akisikika rafiki yake Kasili akizungumza kwa uchungu, kuhusu rafiki yake huyo kujihusisha kimapenzi na mke wake ambaye wamezaa mtoto mmoja.