Jumanne , 5th Feb , 2019

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro leo Februari 5, 2019 amefanya mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa polisi nchini.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amehamishiwa makao makuu ya jeshi hilo na nafasi yake kuzibwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Muliro.

Taarifa iliyoyolewa leo na msemaji wa jeshi hilo, Ahmed Msangi imesema mabadiliko hayo ni ya kiutendaji na kueleza kuwa nafasi ya Muliro imechukuliwa na ACP Mussa Athuman Taibu.

Kabla ya kuwa Kamanda wa Polisi jijini Mwanza Shanna, alikuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Pwani huku Mussa Taibu amewahi kuwa Kamanda wa Polisi jijini Mbeya, kabla ya kurejeshwa Makao makuu ya Polisi jijini Dar es salaam ameteuliwa kuiongoza Kinondoni.