Jumatano , 10th Jul , 2019

Baada ya mahusiano mazuri ya kiuchumi kati Tanzania na China,  serikali kupitia  wizara ya elimu  sayansi na Teknolojia imeona umuhimu wa matumizi ya  lugha ya kichina hapa nchini.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Avemalia Semakafu na Mwalimu idara ya elimu ya sanyansi nchini China He yozhou.

Hilo limebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Avemalia Semakafu, amabapo ameeleza kuwa serikali imeamua kuifundisha lugha hiyo shuleni na vyuoni, ambapo kwa mwaka huu shule 16 zinatarajia kufanya mtihani wa taifa wa  lugha ya Kichina.

Akiongea katika uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya Kichina  chuo kikuu cha Kiisilamu Morogoro (MUM), Semakafu amesema, ''Tanzania kufundisha lugha ya kichina ni muendelezo wa kuimarisha mahusiano yaliyokuwepo hapo awali toka kipindi cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere na kituo hiki kitakuwa  cha tatu kati ya vituo vitakavyokuwa vinafundisha lugha hii ikiwemo chuo kikuu cha Dodoma na chuo kikuu cha Dar es salaam''.

Kwa upande wake Mwalimu idara ya elimu ya sanyansi nchini China He yozhou, amesema mbali na Tanzania na China kushirikiana kiuchumi wameongeza ushirikiano kwenye lugha, ambapo mpaka sasa China imetoa walimu zaidi ya 130 ili waje Tanzania kufundisha lugha ya kichina.