Alhamisi , 20th Oct , 2022

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza Ramadhani Ng 'anzi kuwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania

Na aliyekuwa Mkuu wa Kikosi hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mtafungwa ameteuliwa  kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza

Aidha IGP Wambura amempangia Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei, kuwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi Wasaidizi na Kampuni Binafsi za Ulinzi  nchini  ambapo anachukuwa nafasi ya Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Issack Katamiti.

Katika Uteuzi huo aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Kipolisi Rufiji Kamishna  Msaidizi  wa Polisi (ACP) Protus Mutayoba, amekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rufiji baada ya Kamanda wa Mkoa huo kuhamishiwa Mkoa wa Kipolisi Temeke hivi karibuni.