Jumatano , 25th Mar , 2020

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema leo Machi 25, 2020, amesomewa mashtaka 15 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida, likiwemo la kusababisha taharuki na mengine 14 ya kupotosha jamii.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Mashtaka hayo yamesomwa na mawakili wa Serikali Rose Cholongola, Michael Ngh'oboko, Caren Malando na Monica Mbogo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Consolatha Singano, ambapo imedaiwa kuwa makosa hayo aliyatenda Februari 29, katika mazishi ya kiongozi wa CHADEMA wilayani Manyoni.

Imeelezwa kuwa Februari 29, 2020, Mbunge Lema alisambaza taarifa za upotoshaji kuhusu mauaji ya watu 14 mkoani Singida, ambapo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo alikana na kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 15, 2020 na mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.