Jumatatu , 18th Oct , 2021

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell amefariki dunia kwa matatizo ya kiafya ya Covid-19 akiwa na umri wa miaka 84.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Colin Powell

Jenerali Powell ambaye aliwahi kuwa kamanda wa juu wa jeshi amefariki dunia leo asubuhi kwa mujibu wa familia yake.

Alipanda ngazi hadi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa kwanza Marekani mwenye asili Afrika chini ya Rais George W Bush kwa chama cha Republican.

Wakati akiwa madarakani Powell, aliibua utata baadaye kwa kuhusika kwake kuunga mkono vita dhidi ya Irak.