Jumatano , 16th Mar , 2016

Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa litaendelea kuimarisha ulinzi na usalama hususani kuelekea siku ya uchaguzi jumapili ambapo matukio kadhaa ya kihalifu yameanza kujitokeza ikiwemo kutokea mlipuko nyumbani kwa Kamishna Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omary Makame

Akiongea na Waandishi wa Habari jana visiwani humo Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omary Makame amesema mpaka sasa watu 31 wanashikiliwa na jeshi hilo kuhusiana na ulipuaji wa ofisi za CCM, Mwembekisonge, na matukio wa ulipuaji wa kitu cha afya huku akisema tukio linalomhusu yeye bado wanaendelea kulifanyia uchunguzi.

Aidha Kamishna huyo wa Polisi ametolea ufafanuzi suala la maeneo muhimu ikiweo bandari kulindwa na Wanajeshi hali ambayo inaonyesha kuwatishia baadhi ya wananchi visiwani humo ambapo wengine wameanza kuyakimbia makazi yao.

Kamishna Hamdani ameongeza kuwa jeshi hilo limeongeza ulinzi kwa ushirikiano na jeshi hilo katika kuwasaka wahalifu husussani visiwani pemba ambapo kuna habari za kihalifu zimeripitiwa na kusema kuwa opresheni inayoendelea visiwani pemba ni zoezi la kuwatafuta wahalifu.