Alhamisi , 1st Jan , 2026

Basi la abiria mali ya Kampuni ya Bill Mawio lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Swalehe Adamzi, likitokea Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Msamvu, Morogoro, kuelekea Mkoa wa Tanga, huku lori la mizigo aina ya Howo lenye tela, likitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Mbeya.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania CP Awadhi Haji amefika katika eneo la Gwata Kata ya Mikese Wilaya ya Morogoro, mahali ambapo yamegongana magari mawili kisha yote kuwaka moto jana Desemba 31, 2025 na kusababisha vifo vya watu kumi na majeruhi 23.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Basi la abiria mali ya Kampuni ya Bill Mawio lilikuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Swalehe Adamzi, likitokea Kituo cha Mabasi yaendayo mikoani Msamvu, Morogoro, kuelekea Mkoa wa Tanga, huku lori la mizigo aina ya Howo lenye tela, mali ya Kampuni ya Kikori likiwa na shehena ya mbolea likitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Mbeya.

Waliofariki dunia ni abiria wa basi hilo, wakiwemo wanaume wanane na wanawake wawili. Majeruhi ni 18, wanaume tisa na wanawake tisa, ambapo watoto ni watano, kati yao wavulana watatu na wasichana wawili.

Chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni uzembe wa dereva wa lori la mizigo aliyefahamika kwa jina moja la Abuu, mkazi wa Msoga, Chalinze mkoani Pwani, anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 26 hadi 28