Jumatatu , 27th Jan , 2020

Januari 23, 2020, tulishuhudia Rais Magufuli akimteua Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene, kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, baada ya kumtumbua aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo na Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola.

Mawaziri wa Mambo ya Ndani

EATV na EA radio Digital, imekuletea baadhi ya Mawaziri wa Mambo ya Ndani, ambao wamebahatika kufanya kazi ndani ya Serikali ya awamu ya tano.

Wakati Rais Magufuli anaunda Baraza la Mawaziri kwa mara ya kwanza, alimteua Mbunge wa Misungwi Charles Kitwanga kuongoza Wizara hiyo kuanzia 2015 hadi 2016, lakini baadaye alienguliwa kutokana na kosa la kuingia bungeni akiwa amelewa.

Juni 11, 2016, Rais Magufuli alimteua Mbunge wa Iramba, Mwigulu Nchemba kushika nafasi hiyo ya Charles Kitwanga, akitokea Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuanzia 2016 hadi 2018.

Julai 2018 Rais Magufuli alimuondoa Mwigulu Nchemba katika Wizara ya Mambo ya Ndani, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Baada ya kumuengua Mwigulu Nchemba , Rais Magufuli alimteua Kangi Lugola ambaye alihudumu kwenye nafasi hiyo hadi Januari 23, 2020, na alimuondoa kwa sababu ya kusaini mkataba wa zaidi Trilioni moja.