JPM atoa maelekezo mapya kuhusu Corona

Jumapili , 22nd Mar , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa kuanzia kesho, watu wote wataoingia nchini kutoka katika Mataifa yaliyoathirika na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona watawekwa karantini kwa gharama zao wenyewe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ameyabainisha hayo leo Machi 22, 2020, wakati akilihutubia Taifa kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo nchini, ambapo hadi sasa Tanzania imefikisha visa vya wagonjwa 12 walioambukizwa na virusi hivyo, wanne wakiwa ni raia wa kigeni na nane ni Watanzania.

"Kuanzia kesho, wasafiri watakaoingia nchini kutoka nchi zilizoathirika zaidi na virusi vya Corona, watalazimika kupelekwa katika maeneo maalum kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe" amesema Rais Magufuli.