
1. Donald J. Trump – Rais wa 47 kwenye Taifa la Marekani, mbali na kuzaliwa kwenye utajiri wa kupindukia haikumfanya yeye ashindwe kujihusisha na biashara na kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa ‘’Real Estate’’ kupitia kampuni yake ya Trump Organization
2. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Tanzania, akikaa madarakani kuanzia 2005 hadi 2015. Kabla ya siasa alihudumu kama Luteni Kanali katika Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ)
3. Vladimir Putin Rais wa sasa wa Taifa la Urusi, ametumika kwa miaka 16 kama jasusi kwenye shirika la ujasusi la Urusi (KGB) kabla ya kuingia kwenye siasa rasmi mwaka 1991.
4. Volodymyr Zelenskyy Rais wa sasa wa Taifa la Ukraine, mbali na kuwa na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Kryvyi Rih lakini aliona fursa zaidi kwenye uchekashaji na kujizolea umaarufu mkubwa upande huu kabla ya kuingia kwenye siasa.
5. William Ruto Baada ya kuhitimu mwaka 1990 katika chuo cha Nairobi alifanikiwa kupata Ajira North Rift region of Kenya akiwa kama Mwalimu kwa muda mchache 1990 mpaka 1992 huku akiichapa Injili ipasavyo na kuingia kwenye siasa baadae.
6. Paul Kagame Rais wa sasa wa Rwanda mbali na yeye kusoma chuo cha Makerere Uganda, Lakini pia alifanikiwa kuwa mkuu wa upelelezi chini ya Rais Yoweri Museveni alirudi Rwanda akapigania nchi yake mwaka 2000 akafanikiwa kuwa Rais wa Taifa hilo.