Ijumaa , 17th Sep , 2021

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amempokea kada wa Chama cha ACT-Wazalendo  aliyekuwa mgombea wa ubunge katika jimbo la Kasulu vijijini Edibily Kazala.

Aliyekuwa kada wa ACT Wazalendo Edibily Kazala, akipokea kadi ya uanachama wa CCM kutoka kwa Waziri MKuu Kassim Majaliwa

Akizungumza baada ya kupokea kadi ya CCM, Edibily amesema kuwa ameamua kujiunga na CCM ili kuweza kushikiri kikamilifu katika ujenzi wa Taifa kwa kuunga mkono juhudi mbalimbali za kuleta maendeleo zinazotekelezwa na serikali ya chama hicho.

Amesema kuwa atashirikiana na wanachama wa CCM katika kuhakikisha juhudi za kuwafikishia Watanzania maendeleo zinatekelezwa kama ilivyokusudiwa na chama hicho.