Jumatatu , 14th Jul , 2014

Sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL), kutuhumiwa kuchota fedha katika akaunti ya Escrow, limechukua sura mpya baada ya kampuni hiyo kuamua kumshtaki mahakamani Mbunge wa Kigoma Kusini mhe. David Kafulila.

Msemaji wa chama cha NCCR Mageuzi ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila.

Katika kesio hiyo walalamikaji wamefungua mashtaka wakidai fidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni mia tatu na kumi (310).

IPTL kwa kushirikiana na Kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited na Mtendaji Mkuu wa kampuni hizo, Harbinder Sign Seth, wamemburuta Kafulila katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, na kumfungulia kesi ya madai kutokana na kashfa anazodaiwa kuzitoa juu ya kuchotwa fedha katika akaunti ya Escow isivyo halali.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani, walalamikaji kwa pamoja wameiomba mahakama kuu imwamuru mbunge huyo awalipe shilingi bilioni 210 kama fidia kutokana na kashfa hizo na hasara ya taswira ya biashara ya kampuni hiyo.

Aidha wameiomba mahakama hiyo hiyo imwamwuru mdaiwa awalipe fedha shilingi bilioni mia moja, kama fidia ya madhara ya jumla kutokana na usumbufu walioupata kutokana na taarifa za kashfa dhidi yao.