Ijumaa , 20th Mar , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaomba viongozi wa vyama vya siasa nchini, kuungana kwa pamoja katika kipindi hiki ambacho Dunia inapambana na ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda, na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe.

Makonda ameyabainisha hayo leo Machi 20, 2020, na kumtaka kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, kuachana na nia yake ya kuhamasisha mikutano nchi nzima badala yake aungane na Taifa katika kutokomeza janga la ugonjwa wa Corona.

"Niwatake viongozi wa siasa Corona haina chama , nimeona Kaka yangu Mbowe anasema atafanya mikutano ya hadhara nchi nzima, ni vyema kila kiongozi wa chama cha siasa akatumia ushawishi wake kuwaelekeza wanachama na wafuasi wake umuhimu wa kujilinda na ugonjwa wa Corona" amesema Makonda.